An Integrated, Prosperous and Peaceful Africa.

Top Slides

Mwandishi wa habari wa Afrika lazima achukue jukumu la kutoa taarifa sahihi na zenye usawa kuhusu hali halisi ya maendeleo ya Afrika

Mwandishi wa habari wa Afrika lazima achukue jukumu la kutoa taarifa sahihi na zenye usawa kuhusu hali halisi ya maendeleo ya Afrika

Share this page
October 13, 2022

Waandishi wa habari na watayarishaji wa maudhui ya vipindi barani Afrika wamesisitizwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa ufafanuzi sahihi wa taarifa za Afrika na kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063.

Ili kufanya hivyo, waandishi wa habari wanapaswa kuongeza uelewa wao kuhusu Umoja wa Afrika, sera na maamuzi yanayomuongoza mwafrika wa kawaida kupata maendeleo, miradi mbalimbali yenye tija kwa bara na kuangalia athari zake pamoja na changamoto zinazolikabili na mbinu zilizopangwa za kupunguza. Ili kuwa katika nafasi ya kuwasilisha taarifa za ukweli kuhusu bara la Afrika.

Kundi la watu 15 linalojumuisha waandishi wa habari na watayarishaji wa maudhui kutoka nchi 14 za Afrika wanashiriki katika mpango wa mafunzo ya mwaka mmoja unaosimamiwa na Umoja wa Afrika -AU na shirika la kimataifa la Ujerumani la Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ).

Katika awamu ya kwanza ya programu, washiriki walipata mafunzo ya muda wa wiki mbili nchini Ujerumani yaliyofanyika kati ya Juni 15 na Julai 1.

Washiriki walihudhuria Mkutano wa kimataifa wa Habari wa Deutsche Welle Global Media Forum ambapo walipata fursa kubadilishana ujuzi na kujifunza kutoka kwa wataalamu wengine wa vyombo vya habari,wanaotoa maamuzi na washawishi katika masuala ya siasa, elimu, utamaduni, mashirika ya kiraia, pamoja na mengine mengi.

Wakiongozwa na wakufunzi na washauri, washiriki wamehamasishwa kutumia njia mpya za kuwasilisha taarifa kuhusu Afrika, wakati bara linapojitahidi kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu taarifa zake katika Ajenda ya 2063.

"Kama watu wa Kiafrika na kama waandishi wa habari au watu wa mawasiliano wa Kiafrika, je, hatuchoki kujibu mara kwa mara kwa hasira wakati wowote tunapoona taarifa hizo mbaya ambazo waandishi hawajisumbui kutaja mafanikio yanayoendelea Afrika?

Ikiwa tumechoka basi swali ni tutafanya nini kuhusu hilo?" aliuliza Musabayana katika hotuba yake, na kuongeza kuwa hakuna mtu atakayesimulia hadithi zetu ikiwa hatutafanya sisi wenyewe.

“Habari ni kichocheo muhimu sana cha maendeleo, na si jukumu la mtu mwingine bali ni jukumu letu sisi wenyewe kuhakikisha kwamba tunajileta katika viwango ambapo tunatoa simulizi zinazochangia simulizi za bara linalojiendesha kwa hatima yake. , bara ambalo linapata mafanikio kwa mujibu wa dira na malengo yake yaliyotajwa, bara ambalo linakabiliwa na changamoto, bila shaka… lakini likiwa na mipango ya kupunguza na kuondokana na changamoto hizo,” aliongeza.

Katika kipindi cha wiki mbili zijazo, wanahabari hao wanatarajiwa kupata mfululizo wa mafunzo ya utayarishaji wa habari kwa njia ya simu, yakifuatiwa na ushirikiano na uongozi wa Umoja wa Afrika, ambao umeandaliwa kwa ajili ya kuwaongezea ujuzi waandishi wa habari na kuwajengea uwezo wa kuwa mstari wa mbele.

kutayarisha upya simulizi kuhusu bara hili na kuchangia katika maendeleo yake.

Ushirika wa Vyombo vya Habari wa AU umeundwa ili kutoa jukwaa la kipekee kwa waandishi wa habari wa Kiafrika na watayarishaji wa maudhui ili kuongeza uwezo wao wa kurekebisha simulizi za Kiafrika na kuhakikisha kwamba hadithi kuhusu bara hili zinasawazishwa na zinaonesha uzoefu wa Waafrika katika njia za kuvutia na za ubunifu.

Imeandikwa na Johnson Kanamugire - 2022 AU Media Fellow

Imetafsiriwa na Esther Namuhisa - Mshiriki wa mafunzo kwa wanahabari wa AU- 2022

Jiunge na mazungumzo kwa kutumia #AUMediaFellowship #AU20

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Bi. Faith Adhiambo, Afisa Mawasiliano- Agenda 2063 Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano | Tume ya Umoja wa Afrika

Simu: +251 115 517 700 | Barua pepe: ochiengj@african-union.org | Addis Ababa, Ethiopia

 Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano, Tume ya Umoja wa Afrika I Barua pepe: DIC@africa-union.org

Topic Resources